Tanzania Nchi Yetu Sote
Dar es Salaam
Katika nchi ya vipofu chongo huwa ni mfalme. Hakika nchi nzuri hujengwa na wazalendo na huliwa na mafisadi, ni jukumu la vijana kuipigania nchi yao isiendelee kuliwa na mafisadi. Kumbuka kura yako moja ina nafasi kubwa sana katika kuamua juu ya mustakabali wa taifa hili. Ukisema hupigi kura unashiriki kwa kiasi kikubwa sana kuachia wajinga wachague viongozi ambao watakuongoza hata wewe pia. Kulalamika bila kuchukua hatua ni kukukubaliana na unayolalamikia.