PATRICK SAID
Evangelist in TANZANIA
Habari! Jina langu naitwa PATRICK SAID ni Mkristo niliyezaliwa mara ya pili katika Kristo Yesu Bwana! aidha mimi ni Mhubiri wa habari njema za ufalme wa Mungu kwa watu wote, Maisha ya wokovu sio maisha ya dini au udhehebu bali ni mabadiliko yanayotokea kwa mtu baada ya kumkubali Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi! ni kama uamuzi wa mwana mpotevu kurudi kwa baba yake Luka 15:11-32, ni uamuzi wa kuacha njia mbaya na kuigeukia njia na mwenendo mpya unaoongozwa na Mungu, maisha haya ni maisha yenye amani timilifu ambayo huwezi kuipata katika ulimwengu wala katika anasa na starehe bali katika Kristo Yesu Bwana aliye Amani yetu, Ni katika kuzaliwa mara ya pili pekee mwanadamu anapata nafasi ya upendeleo yaani Neema ya kuingia katika ufalme wa Mungu.
"Yesu akajibu akamwambia amin amin nakuambia mtu asipozaliwa mara ya pili hawezi kuuona ufalme wa Mungu" Yohane 3:3
Rafiki unahitaji kufanya maamuzi ya kufungua mlango wa moyo wako kwa Mungu kwa kumkubali Bwana Yesu aliye Njia, Kweli na Uzima, ili kwa Nguvu na uweza wa Roho Mtakatifu uzaliwe upya katika Kristo Yesu na kuwa mwana wa Mungu, neema hii ni ya bure kabisa wala haihitaji gharama yoyote zaidi ya maamuzi yako kwani gharama yote imelipiwa msalabani na Bwana Yesu kwa Damu yake ya thamani! Ipo furaha kubwa sana Mbinguni mwenye dhambi mmoja atubupo! unapoikataa neema hii unajihukumu moja kwa moja. Kama umeguswa na upo tayari kutua mzigo wa dhambi zako msalabani ambapo Bwana Yesu alichukua dhambi zetu, madhaifu yetu na Magonjwa ili atuhamishe kabisa kutoka ufalme wa giza na kutuingiza katika ufalme wa mwana wa pendo lake tafadhali bofya kitufe "CONTACT ME" Hapo chini👇, aidha kama una maswali zaidi na unatamani kujua zaidi juu ya habari za Yesu tumia kitufe hicho.
Mungu akubariki!